34 views
3mo ago General
Mahakama kuu imewaagiza maspika wa bunge la taifa na seneti kutojihusisha na shughuli za kisiasa kufuatia rufaa iliyowasilishwa na kundi la Vocal Africa. Jaji wa mahakama kuu David Mburu leo alitoa agizo linalowazuia wawili hao kutumia nyadhifa zao kuhimiza siasa za upande mmoja, au ushawishi wa nyadhifa zao kuandaa, kuendesha au kushiriki kampeni za kisiasa. Agizo hilo litadumishwa hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa. Mwanahabari wetu wa masuala ya mahakama, Ruth Wamboi anatuarifu zaidi.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive